Somo la kumi na mbili

Hii ni biashara ya akili sababu unatakiwa kuchukua faida kutoka kwa watu ambao ni smart, ambao wanajitahidi sana kuchukua pesa kutoka kwako pia 😊

Hivo kila trade ni kubwa na ngumu. Hakuna trade rahisi.

MITAZAMO AMBAYO ITAKUONGOZA SOKONI.

1. Kuwa na mtazamo wa kuwa market itaendelea kufanya kitu ambacho imekua ikikifanya siku zote.

2. Soko linapokua lipo kwenye uelekeo imara, 80% ya majaribio ya kuligeuza huwa yanafail (hivo trade kulingana na uelekeo husika)

3. Pindi market ikiwa kwenye Trading Range, 80% ya majaribio ya kurudi kwenye trend husika huwa yanafail (Hivo trade kinyume na uelekeo wa trend hio)

KEY TO YOUR SUCCESS 

Kuna kanuni tano ambazo ninatamani kushare jioni ya leo na wewe. Kwa kuzifuatilia kanuni hizi utajiengua kutoka kwenye maelfu ya trader ambao kwao trade ni kama kamali. Hivo soko la Forex na michezo ya kubet ni vitu viwili tofauti sana kwa traders ambae atafuata kanuni hizi.


1. MPANGO MKAKATI 
Watu wengi ambao wamefanikiwa kwenye mambo mbalimbali, walikua na mkakati fulani walioundaa ambao baada ya kuufuata umewafikisha pale ambapo wapo. Hata traders waliofanikiwa katika trading pia huwa na mikakati ambayo hufuata. Unatakiwa kuwa na mfumo wako ambao utakuongoza. Ratiba, muundo au ramani. Mpango wako unaweza uwe rahisi au wenye maelezo ya undani, lakini lazima uwepo. Swali la kukuanziashia mpando mkakati ni “KWANINI UNATRADE!?”


2. MAFUNZO 

Kuna watu wanatumia signal kwa ajili ya kutrade. Lakini unatakiwa kupata mafunzo ambayo yatakupa uwezo wa kuchambua na kuona fursa wewe binafsi. Hakikisha unaelewa kila stategy ambayo utaenda kuitumia. Kuwa nguli wa hio strategy na elewa undani wake nje ndani. Kama umefanikiwa kusoma kuanzia kule juu. Kanuni hii kwako tayari umeshaifikia 80% .


3. VIFAA/ VITENDEA KAZI. 

Kwa mazingira halisi ya kufanya trading vifaa vya kufanyia kazi ni muhimu sana. Hio ndio ofisi yako. Moja ya vitu vya msingi sana kwa mtu anayeanza ni namna gani atatumia application za kufanyia trading. Na niliweka namna ya kutumia trading view kama moja ya site ambayo itakusaidia katika ufanyaji wa analysis. 
Lakini ubora wa Simu au laptop yako ni muhimu sana katika biashara. Hautakua na trade ya amani kama simu au laptop yako unavyoitumia inakupa headache. Mtandao mbovu au umeme ukikatika saa 1 moja simu yako na laptop yako vinazima pia. Unaweza kuwa mwelevu, una maarifa ya kutosha lakini uhaba au uhafifu wa vifaa vizuri ukakurudisha nyuma.

Kwenye hii biashara kuwa na simu ya millioni mbili au laptop ya millioni mbili sio anasa bali ni uboreshaji was mqzingira ya kazi. Huwezi kuwaza kutengeneza millioni 10 au hamsini kwa mwezi kwa kutumia kifaa cha laki na hamsini au laki mbili.


4. NIDHAMU 

Hofu na matamanio ni moja ya sifa za ubinadamu. Vitu hivi vinaweza kuwa vikwazo katika safari yako ya trading kama hautakua na sheria za kuvidhibiti hivi vitu viwili. Trading sio ngumu kama vile ambavyo tunataka kujiaminisha. Unatakiwa kufanya maamuzi sahihi ya kusimamia trades ambazo zipo upande sahihi ili ziendelee kukupa mafanikio na kuziondoa trade zisizo upande sahihi na hii hufanywa kwa kuweka Stop loss.


5. UTEKELEZAJI

Kwa traders wanaoanza ni sawa kuwa na mkanganyiko wa mawazo ya nini ukisikie na nini ukiache. Hata sisi tumepitia huko kujaribu strategy za kila aina mpaka tulivokuja kutulizana. Hata kama kila mtu athubiri kuwa Price Action ndio strategy bora zaidi lakini hii inaweza isifit kwako. Ukajiona kila ukihitaji kuifuata akili yako haitaki kabisa kuelewa. Hio sio kosa ndivyo tumeumbwa kwa utofauti wa interest.

Mfano mimi nilikua natamani sana kusoma Elliot wave. Na nilivofika nafasi fulani nililipia mpaka mentorship kwa watu ambao wanaaminika katika hio strategy lakini ilinishinda mpaka nilipojua kuwa nafit vizuri kwenye price action.

Hivo utekelezaji ukawa kuwa kwenye mkakati wa kuhakikisha naielewa nje ndani Price action na mtu yoyote ambae anafanya Price action namuangalia zaidi. Hii ndo sababu kwenye uchambuzi wa Price action nimefika hapa.

Comments