Somo la kumi na moja


MARKET SESSION 

Tumekua tukisia market inamove masaa 24, Labda mtu anajiuliza kwanini hii inamove hivi au kwanini ni masaa 24. Kumekua na zile Center kubwa duniani ambazo ni maeneo mama ya zile sarafu muhimu ambazo tumeziangalia huko juu. Sasa kutokana na utofauti wa kijografia maeneo haya yammekua na muda tofauti. Leo hii duniani utasikia kukiwa mchana Tanzania, Canada ni usiku. So utofauti huu unafanya maeneo hayo kuwa na muda tofauti wa kurun biashara zao hivo kufanya mgawanyiko wa session katika soko. Hapa chini nakuelezea session hizo;


AUSTRALIAN SESSION (SYDNEY STOCK EXCHANGE) 

Hii ni Australia 🇦🇺, na kulingana na jografia hili ni eneo la kwanza duniani kuona jua/siku mpya. Hata mwaka mpya, Australia huanza kusherekea mwaka mpya kisha maeneo mengine ya dunia hufuata.

Sarafu ambayo ipo katika soko la hisa la Sydney ambao ndio mji mkuu wa Australia ni Dolla ya Australia (AUD) ndo maana katika kalenda ya matukio ya kiuchumi tunaona matukio yake hutangazwa sana usiku.

Australia hufungua shughuli zao za kiuchumi kuanzia Saa 2 asubuhi mpaka saa 10 jioni kwa mda wao. Ambapo kwa muda wa Afrika mashariki ni sawa na saa 6 usiku mpaka saa 2 asubuhi. Ndio maana ikifika saa 6 usiku jumapili soko hufunguliwa kwa huku kwetu hio ni sawa na saa mbili asubuhi jumatatu kwa Australia.

Muda huu pia sarafu ya dolla ya New Zealand pia huwa ipo sokoni kwani ni maeneo ambayo yapo ukanda mmoja.


ASIAN SESSION (TOKYO STOCK EXCHANGE)

Bara la Asia linabebwa na nchi ya Japana katika shughuli za kiuchumi. Hii inatokana na shughuli za kiviwanda ambazo zipo Japana na Centre ya kibiashara kwa nchi za Asia inatajwa kuwa ni Japan. Tokyo ni mji mkuu wa Japan ndio maana hapa tunazungumzia soko la hisa la Tokyo.

Sarafu inayotumika Japan, ni Yen ya Japan (JPY). Japan huanza shughuli zao saa 2 asubuhi mpaka saa 10 jioni kwa mda wao ambao hio ni sawa na Saa 8 usiku mpaka saa nne asubuhi kwa muda wa Afrika mashariki. 

Hiyo ni kumaanisha Tokyo na Sydney zinakutana katika soko kuanzia saa 8 usiku mpaka saa mbili asubuhi ambapo Sydney wanafunga shughuli zao.


EUROPE SESSION ( FRANKFURT STOCK EXCHANGE) 

Ulaya hapa kuna session mbili hii ya FRANKFURT NA LONDON. Sababu ya kuwa na hizi session mbili ni kwa sababu kuna sarafu ambayo inatumiwa na nchi za umoja wa Ulaya ambayo ni Euro na United Kingdom wao wa pound. Hivo ikafanya kuwe kuna mgawanyiko wa session kulingana na hizi sarafu zote kuwa na nguvu. 

Frankfurt huanza shughuli zao za kiuchumi saa 2 asubuhi mpaka saa 10 jioni ambayo hii ni sawa na saa 2 asubuhi mpaka saa 10 jioni ya Afrika mashariki. Hii kutokana na kuwa tupo katika ukanda mmoja. 

So hii ni kumaanisha wakati Sydney wanafunga shughuli zao, Frankfurt wanaanza shughuli zao na wanakua a na Tokyo kuanzia saa mbili mpaka saa 4 asubuhi ambapo Tokyo wanakuwa wamefunga pia. 

Kwenye hii session kuna Swiss Franc pia ya Urusi inakua ipo active.


EUROPE SESSION (LONDON STOCK EXCHANGE) 

Hii ni Uingereza, hapa kama upo opposite na trade zako muda huu ndipo mbivu na mbichi huonekana. London panatajwa kuwa ni moja ya kitovu kikubwa cha biashara duniani. Hivyo soko la hisa la London likiwa wazi market inakua active sana. Kama kulikua na movement ndogo kwenye session nyingine hapa movement huwa kubwa sana.

London huanza shughuli zao za kiuchumi saa 2 asubuhi mpaka saa kumi jioni ambayo ni sawa na saa 4 asubuhi mpaka saa 12 jioni kwa muda wa Afrika mashariki. Hiyo ni kumaanisha wakati Tokyo wanafunga shughuli zao, London wanafungua shughuli zao na kukutana na Frankfurt na nchi nyingine za ulaya mpaka saa 10 jioni ambapo Frankfurt hufunga soko lake.


AMERICA SESSION (NEW YORK STOCK EXCHANGE)

Hii ni marekani huko, session ya Mwisho kwenye soko. Huanza saa 2 mpaka 10 jioni kwa muda wao ambao ni sawa na saa 9 alasiri mpaka saa saa 6 usiku kwa muda wa afrika mashariki. Hiyo ni kumaanisha wanakutana na Frankfurt mpaka saa 10, kisha Frankfurt wanafunga na wana endelea na London mpaka saa 12 ambapo London hufunga soko Lao kisha Marekani wanaenda mpaka saa 6 usiku ambapo mda huo ni siku ya pili kwa Australia wanafungua soko lao.

Marekani wanaonekana wanakua wapo sokoni mpaka saa 6 kutoka saa 9 mtu atajiuliza mbona wanazidi masaa 8. Yes, hii inatokana na ukubwa wa marekani kwani New York inavokua saa 2 asubuhi maeneo mengine kama Chicago, Los angeles huwa nyuma kwa saa 1 au mawili. 

Kwenye hii session pia kuna sarafu ya dolla ya Canada pia huwa active (CAD).


NB: Haimaanishi eneo likifungwa na sarafu yake inakuwa haifanyi kazi sokoni. Mwana FA anakwambia pesa hailali unalala wewe. Leo tukienda kwenye kubadilisha fedha kwenye soko la hisa Dar es salaam. Ukitaka dolla ya marekani unaipata lakini sasa hivi marekani ni usiku wamelala. Hivo masoko yanafungwa lakini sarafu zao hazilali sababu bado zinatumika maeneo mengine.

Comments