Somo la kumi

CHART PATTERNS 

Kwenye trader ambao tunatumia strategy ya price action, Macho yako na uwezo wa kutafsiri chati ndio utajiri wako. Chati zetu huwa tupu hivyo vitu kama Resistance na Support, Trendline, candlestick pattern na charts ni vitu ambavyo wewe binafsi ndio unatakiwa kudevelop.

Tofauti na watu ambao hutumia indicator, ambapo huongozwa na hizo indicator kupata picha ya soko. Hasara ni kuwa unahitaji mazoezi ya mara kwa mara kuizoea chati ili uweze kuona vitu tofauti kwenye soko. Na Faida ni kuwa utaweza kuwa mbele kwenye ufanyaji wa maamuzi kuliko watu wa indicators sababu watu wa indicator husubiri mpaka indicator idevelop hali ambayo mara nyingi market inakua ishafanya movement. 

Hapa chini nimekuandalia chart patterns maarufu ambazo hizi hutupatia ishara ya jambo ambalo litaenda kutokea mbele.

1. RECTANGLE BOX 

Hii ni mapumziko ya safari ya price kwenye soko. Mara nyingi huwa tunasema ni nusu ya safari ambayo price inatarajia kutembea. Rectangle hutokea baada ya movement ya price kisha price inapumua ili iendelee na safari. Inawezekana price ikaweka mapumziko ya kwenda juu (bullish) au mapumziko ya kwenda chini (Bearish). Tazama picha hapo chini

2. BULL FLAG 

Hii pia ni pattern ambayo huonesha kupumzika kwa movement ya price kwa mtindo wa kurudi nyuma lakini ikiwa ndani ya wigo/mkondo fulani. Mara nyingi pattern hii tunaiobserve kwa kuilabel kwa kama channel. Baada ya safari ya kupanda market inatafuta nguvu ya kupanda zaidi kwa kurudi hatua kadhaa nyuma. Hii hutokea wakati wa bullish movement kwenye soko. Angalia picha hapo chini


3. BEAR FLAG 

Hii ni kinyume cha bull flag. Inakua na sifa zote nilizoeleza kwenye bull flag tofauti yake hii hutokea market inapokua inashuka chini. Tazama picha

4. RISING WEDGE 

Hii hutokea kama reversal kutoka bullish movement kwenda bearish movement. Movement inakua inapoteza nguvu kadri inavyopanda juu na kutengeneza pembetatu ncha (kiswahili bhana- Sharp triangle) hivyo pindi ikivunja upande wa chini inakua ni kiashiria cha kusell.

5. FALLING WEDGE 

Hii hutokea kama reversal kutoka bearish movement kwenda bullish movement. Movement inakua kama inaongezeka upana kadri inavyoshuka chini na kutengeneza pembe tatu muachano 😅. Kuna rafiki yangu mmoja alitumia mfano wa mtu akianza kufanikiwa anaanza kuvimba. Hivyo hapa market inaanza kuvimba sababu inataka kwenda juu 😂. Tazama mfano wa picha hapa chini


Comments