TYPES OF TRADER
ukishaanza kutrade kulingana na kiasi cha uvumilivu na mihemko yako utajikuta mnaanza kutofautiana na watu ambao wamekuzunguka kuhusu aina ya kufanya trading . Kuna watu hupenda vitu vikubwa kwa haraka na kuna watu huamini katika kidogo kidogo katika longterm, na hii ndio inatugroup matrader katika makundi manne tofauti.
Makundi haya ni;
1. SCALPING
Hii ni aina ya trader inayofanywa kwa kukaa kwenye trade ndani ya muda mfupi na kutoka. Trader wa scalping hukaa kwenye trades ndani ya dakika moja mpaka tano. Pindi ambapo kuna fundamental factor yoyote imekua released price hutembea kwa haraka sana mda huo kabla haijaendelea na movement ya kawaida hivo wakati huu ndipo fundamental traders huutumia. Scalpers daima hutumia Timeframe za dakika moja 1M TF na dakika tano 5M TF
2. INTRADAY/DAY TRADING
Hili ni kundi la traders ambao hufanya trades zao ndani ya siku husika bila kulala na trade ikiwa inarun. Huamka asubuhi na malengo fulani ambayo yakikamilika siku yao imekamilika. Hii ni sehemu ambayo ina matrader wengi zaidi kuliko kundi lolote. Kundi hili hufanywa na watu wa rika zote. Timefame wanazotumia kundi hili ni dakika kumi na tano 15M TF , dakika thelathini 30M TF na saa moja 1Hr TF.
3. SWINGING
Hii ni aina ya trade ambapo trades hulala kwa siku zaidi ya moja zikiwa zinarun. Mara nyingi swingers hutumia timeframe ya masaa manne 4Hr TF na siku moja 1D TF. Target za swingers huanzia pips 50 kwa trades moja mpaka pips 500 kulingana na mwenendo wa pair husika. Aina hii ya trades inatamkwa kuwa ni aina ya wale traders wenye uzoefu na wamekua matured kwenye soko.
4. POSITION TRADERS
Hili ni kundi dogo sana. Watu/Trader ambao wameshakuwa matured enough kwenye tradings hawa ndio huwa kwenye kundi hili. Hii inahusisha kuhold trades moja kwa zaidi ya wiki au mwezi.
Hurisk kiasi kidogo ambapo hutegemea pips nyingi zaidi!
Takwimu huonesha candlestick ya mwezi katika pair hutembea kwa pips zisizopungua 1000 !
Hivo kama mtu ana $100 kisha akapata trades 5 kwa mwezi ambazo zitatembea kwa pips 1000 kila moja kwa kutumia lotsize ya 0.01. Ana possibilities ya kupata faida ya pips 5000 kwa mwezi ambapo kwa 0.01 ni sawa na $500 toka kwenye mtaji wa $100. Lakini kama nilivosema huu ni mfano 😃😃.
Comments
Post a Comment