PIP/ PIPS
Tunachokitrade kwenye forex ni movement au tofauti ya bei kutoka pointi moja mpaka nyingine. Na kipimo ambacho kinatumika kupima tofauti hio au kutambua tofauti hio huitwa PIPS. Tunaposema GBPUSD imepanda toka pointi A mpaka pointi B , kipimo cha pointi A mpaka B ni Pips ndipo tutajua imetembea kwa pips ngapi.
Hivyo tunachokitafuta kwenye market all day ni pips.
TAKE PROFIT
Baada ya kuuza au kununua katika soko hauna haja ya kukaa kwenye chart unaitizama ifike idadi ya pips unazohitaji, Hivyo utaweka oda ya kujifunga pindi price au somo litakavyofika kwenye pips unaohitaji kama faida, Oda hio au hilo eneo huita Take profit
STOP LOSS
Unavyotrade lazima ujue katika hii trade yangu kama market haitaenda kama nilivyotarajia basi ikifika eneo hili trade hii itakua ni invalid. Eneo ambalo trade yako unaona ikifika trades hio itakua Invalid eneo hilo linaitwa STOP LOSS. Eneo ambalo ni ukomo wa hasara isiendelee.
LOTSIZE
Baada ya kujua kwamba tunachotrade kwenye market ni movement na faida ni pips kuna mtu anajiuliza napataje hela sasa 😂.
Well! Ni hivi faida ya hela utakayopata itategemea na lotsize ambayo utatumi kutrade!
Kama umeona picha mbalimbali za trades utaona buy then mbele kuna vinamba kisha faida au hasara vile vinamba ndio lotsize.
Angalia mfano hapo chini


Comments
Post a Comment