MISAMIATI MUHIMU KWENYE KUTRADE.
Kabla hatujaanza kuanza kusoma namna ya kufanya uchambuzi hebu tuangalie misamiati mbalimbali ambayo wenzetu waliotutangulia kujua skills wanatusumbua nayo mtaani, Tunaonekana wakuja sana 😅. Hapa chini naielezea misamiati hio
BULL/BULLISH/LONG
Bullish imekua originated toka kwenye neno Bull. Huyu ni ng’ombe dume. Ambapo akitaka kukudhuru akakuchota na pembe zake kisha anakurusha juu. Hivyo kwenye market kukiwa kuna bull/bullish movement maana yake market inatoka chini inaenda juu. Na pindi ambapo kunakua na movement hii order inayotakiwa kuwekwa kwenye market ni Buy au wengine huita long. Kwa sababu Bulls wanakula majani hivo candlestick itakayoonesha taswira ya movement ya bullish huoneshwa kwa rangi ya kijani.
NB: Maelezo ya candlestick yanafuata
BEAR/BEARISH/SHORT
Bearish imekua originated toka kwenye neno Bear. Huyu ni mbwa wa porini au kwa jina la kiswahili anaitwa dubu, ambapo akitaka kukudhuru anakurukia juu kisha anakupeleka chini. Hivyo kwenye market kukiwa na bear/bearish movement maana yake market inamove kutoka juu kwenda chini. Na pindi kunavokua na movement hii order ambayo inayotakiwa kuwekwa kwenye market ni Sell au wengine huota Short. Kwa sababu Dubu/bear anakula nyama hivyo Candlestick itakayoonesha taswira ya bearish huoneshwa kwa rangi nyekundu.
CANDLESTICK
Hii ni bar ambazo zipo kwenye chart zinazotumika kutuonesha price ilivyofanya katika muda fulani uliopita. Bearish candlestick huwa ya nyekundu au nyeusi, na bullish candlestick huwa kijani au nyeupe. Hatuwezi iita Candlestick fulani bearish au bullish kama bado haijaclose kwani jambo lolote linaweza kutokea.
SELL/ SHORT
Hii ni oda ambayo unaweka kwenye market unapoamini kwamba market itaelekea chini. Tunauza kwenye pointi ya juu ya bei ili ikifika pointi ya chini tufunge, kisha tofauti ya tulipouza na pale tulipofunga ndio faida yetu in terms on Pips
BUY/LONG
Hii ni oda ambayo unaweka kwenye market unapoamini kwamba market itaelekea juu. Tunanunua kwenye pointi ya chini ya bei ili ikifika pointi ya juu tufunge, Kisha tofauti ya tuliponunua na tulipouzia ndio faida yetu in terms of pips

Comments
Post a Comment