Somo la tatu

ANALYSIS 


Uchambuzi katika soko ndio kitu kinachotusaidia kujua uelekeo wa soko kua linaenda wapi. Baada ya kufanya uchambuzi tunakua na jibu kamili kuwa tutegemee uelekeo huu kulingana na historia au taarifa zilizopita. 

Uchambuzi umegawanyika katika makundi matatu.

1. FUNDAMENTAL ANALYSIS

Huu ni uchambuzi unaotokana na kufuatilia taarifa za kiuchumi, kisiasa, kijamii na kidiplomasia ambazo hupelekea kuathiri sarafu kwa matokeo chanya au negative. 

Matukio mbalimbali yenye uzito duniani yanapotangazwa huathiri mwenendo wa sarafu husika au soko zima. Hapo juu nimeeleza kuwa dolla ya marekani ni major currency hivyo kama kuna tukio litaathiri sarafu hii basi tunatarajia kuona mabadiliko makubwa sokoni. Mfani hii vita ya kiuchumi baina ya China na Marekani inayoendelea sasa. Trader wengi wamekua wakicomment Donald Trump anahitaji kukua 😃. Hivyo kuna matrader au institution ambazo hufanya analysis kwa matukio haya. Mfano Wall Street marekani. Au trade wengi ambao huscalp hutegemea kalenda ya matukio haya ili kufanya scalping (Tutaona hapo mbele scalping ni nini)

2. SENTIMENTAL ANALYSIS 

Uchambuzi huu ni ile hali ya kuchambua, kulinganisha na kudadavua taarifa fulani zilizotolewa au ambazo zipo ili kufanyia maamuzi. 
Mfano leo trader anaweza akawa amemfollow Carlos Kapinga wa FEA pamoja na Prince wa PipsKing. Kisha anakusanya taarifa za hawa matrader wawili kisha anakuja na mawazo binafsi kulingana na taarifa alizozipata sehemu hizo mbili. 

Sizani kama hii ni aina bora sana ya uchambuzi kufanywa na mtu ambae ameweka mtaji wake alioupata kwa shida ili atengeneze faida.

3. TECHNICAL ANALYSIS 

HIi ndio hasa hata mimi nipo hapa. Uchambuzi wa kusoma tabia ya sarafu ilifanyaa nini wakati uliopita ili kupredict itafanya nini katika nyakati zijazo. Hapa panakuisha;

1. Price action ( chart patterns, zones, Candlestick Patterns)

2. Naked chart- Chart tupu ambayo inakua na picha ya structure ambazo wewe ndo unaziobserve kama last kiss big shadow nk 

3. Indicators- hizi ni programing software ambazo huonesha viashiria kulingana na historia ya price ambqzo hufanya. Mfano Moving average, Bollinger bands, Stochatic Oscillator nk 

Hapa tutajikita zaidi katika application na baadhi ya vitu kwenye naked chart.

Comments